Leo Desemba Mosi, 2016 mwili wa marehemu Mzee Xavery Pinda ambaye ni baba mzazi wa Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda anazikwa katika kijiji cha Kibaoni wilaya ya Mlele mkoani Katavi.

Mzee Xavery alifariki dunia Novemba 27, 2016 saa 9.30 alasiri katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma alikokuwa amelazwa akipatiwa matibabu.

Akizungumza wakati wa kuaga mwili huo nyumbani kwa Pinda kijijini Zuzu, Manispaa ya Dodoma  leo Novemba 30, 2016 Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete amesema marehemu Mzee Xavery alikuwa mwema sana na alikuwa na upendo kwa watu wote. Amesema anamkumbuka sana kwani alikuwa rafiki yake aliyewahi hata kumpa zawadi ya kuku wakati alipokuwa rais.

Wizara ya elimu yatoa ufafanuzi kufungia kozi za kujiongzea uwezo
Rais Magufuli atoboa siri ya kuteua wanajeshi Serikalini