Aliyekuwa mchezaji wa klabu ya Simba zamani, Abdallah Kibadeni amefunguka kero yake kubwa kwenye klabu za mpira za sasa hapa nchini ambazo ni watani wa jadi Simba na Yanga na kusema kuwa inamuuma sana kuona viongozi wa hizi klabu kusajili idadi kubwa ya wachezaji wageni kuchezea klabu hizo na kuwaacha vijana wazalendo wenye vipaji wa hapa nchini.

”Nafarijika na ushabiki lakini kinachoniuma wachezaji tunaowatumia sana wageni wa nje na hiyo sio sawa” Kibadeni

Hivyo ameomba iwepo nguvu ya kuwashawishi viongozi hao kuacha tabia ya kuwategemea wachezaji wageni na kusisitiza kuwa ni vyema kuwatumia wachezaji wetu wazawa kwani kwa sasa mpira ni ajira na biashara ambapo watu wakubwa wenye fedha zao wanawekeza humo.

‘Timu zinatawaliwa na wageni zamani ukitazama simba ukitizama yanga unakuta watoto wote wanaochezea hizi timu ni watoto wanaojulikana na wazazi wao wanajulikana, ile imeondoka sababu mpira saivi ni biashara hata ushindani umekuwa mdogo sana” amesema Kibadeni.

Ameongezea ”Tuwatumie wachezaji wetu wazawa tuhakikishe wazazi mnahakikisha wototo wenu wanacheza mpira kwa sasa ni biashara”.

Amesema kuwa kwa sasa biashara imekuwa nyingi na ushindani umepungua kulinganisha na miaka ya nyuma mabapo ushindani, utani na uzalendo ulikuwa mkubwa.

”Sasahivi biashara imekuwa nyingi na ushindani umepungua, utani wa jadi ulikwepo sasa ivi mtu leo anafungwa kesho anatembea, anaenda dansi miaka yetu simba na yanga kwa mwaka ilikuwa inacheza mara moja, timu inayofungwa inavaa kitambaa cheusi mwaka mzima mpaka itakapo funga tena”.

Aidha katika kikosi cha Simba pekee idadi ya wachezaji wageni yapata 10, ambapo kati ya hao wachezaji 7 hupata nafasi ya kuingia katika kikosi cha kwanza cha mashumbulizi uwanjani, huku upande wa Yanga wachezaje wageni wafikia idadi ya 10 pia.

 

Kenya kuwarudisha nchini wanafunzi 85 waliopo China
Video: HARMONIZE anaweza kuishiwa muda si mrefu? |Video mpya ya MARIOO YAIBUA ajabu lingine