Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Jumanne Murilo amesema kuwa kwasasa mkoa huo uko shwari ukilinganisha na kipindi cha nyuma.

Ameyasema hayo alipokuwa akizungumza Dar24 Media, ambapo amebainisha kuwa kwasasa hali ni nzuri na matukio ya uhalifu yamepungua.

Amesema ukilinganisha kipindi cha nyuma na sasa kuna mabadiliko makubwa zaidi kwani kwasasa imekuwa ni adimu kutokea kwa matukio ya kihalifu.

“Kwasasa hali ni shwari ukilinganisha na hapo awali, Jeshi la polisi kwa kushirikiana na idara mbalimbali limejipanga vizuri kuhakikisha linatokomeza uhalifu,”amesema Kamanda Murilo

Walawiti 6 washikiliwa na polisi
Video: Vurugu polisi ikituhumiwa mauaji kijana, Magufuli awapa neno maaskofu

Comments

comments