Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amezindua kitabu kinachotoa muongozo na taratibu za kufuata wakati wadau mbalimbali wanapotaka kujenga viwanda kuanzia ngazi ya kijiji hadi mkoa.

Uzinduzi huo umefanyika wakati akifungua Maonesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar-es-salaam katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, ambapo amesema lengo la mwongozo huo ni kujenga uelewa wa pamoja kwa wadau wa viwanda nchi nzima.

“Kijitabu hiki kidogo kina maelezo muhimu kuhusu taratibu za kufuata unapotaka kujenga kiwanda, kuanzia kutenga maeneo ya kuvutia uwekezaji na hata kuendesha makongamano ya biashara,”.

Aidha, amewashuru na kuwapongeza washiriki wote wakiwemo wa sekta binafsi kwa ushiriki wao. Amesema kwamba Serikali inatambua kuwa sekta binafsi ndio muhimili mkuu wa kujenga uchumi wa viwanda nchini.

Pia, Waziri Mkuu amegawa tuzo kwa washiriki mbalimbali wa maonesho hayo, ambapo Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) limeibuka mshindi wa jumla.

Baada ya kufungua maonesho hayo, Waziri Mkuu alitembelea mabanda mbalimbali yakiwemo ya Zanzibar, Viwanda na Biashara, Asasi, Azam, TPA na EOTF

Changamoto ya elimu yatajwa zao la Parachichi kukosa ubora Njombe
Video: Mwigulu Nchemba aibuka, Hii ndio inavyotakiwa

Comments

comments