Mabingwa wa Soka Tanzania Bara, Klabu ya Yanga imemtangaza msemaji mpya wa timu hiyo, Dismass Ten kuchukua nafasi ya aliyekuwa msemaji watimu hiyo, Jerry Moro alimaliza mkataba wake.

Jerry Muro ambae alikuwa akitumikia kifungo cha mwaka mmoja alichofungiwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) amemaliza mkataba wake na Klabu hiyo yenye maskani yake jangwani jijini Dar es salaam.

Aidha, Dismas Ten kabla ya kusaini mkataba na Klabu ya Yanga alikuwa msemaji wa timu ya Mbeya City yenye maskani yake jijini Mbeya ambapo kwa sasa ataitumikia Klabu hiyo ya jijini Dar es salaam.

Hata hivyo, kwa upande wake Katibu Mkuu wa Klabu hiyo ametoa pole kwa watani wao Klabu ya Simba kwa kukamatwa viongozi wake na kuwekwa ndani kwa makosa yasiyokuwa na dhamana hivyo kuwataka wanachama na mashabiki wa timu hiyo kuwa wavumilivu kwa kipindi hiki.

Magazeti ya Tanzania leo Julai 15, 2017
TCRA yazikomelea msumari wa moto Kampuni za simu