Mbunge wa Jimbo la Ubungo kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Saed Kubenea amesema kuwa hang’oki ndani ya chama hicho na kujiunga na CCM.

Amesema kuwa kazi ya kumchafua na kumzushia kuwa anataka kuhama chama inafanywa na viongozi ndani ya Chadema ambao amesema wanamalengo yao binafsi.

Ameyasema hayo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema kuwa taarifa hizo ni za uzushi zenye lengo la kumchafua.

“Mimi sijawahi kuzungumza na mtu yeyote wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kwa hiyo taarifa zinazozagaa kwenye mitandao sio za kweli, na zinafanywa na baadhi ya viongozi ndani ya Chadema na wanafahamika, sasa mimi nawaambia Chadema sing’oki,”amesema Kubenea

 

Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Julai 31, 2018
Ndugai anena kuhusu Waitara, sasa kuiandikia barua NEC