Mgombea wa kiti cha Ubunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wa Jimbo la Kinondoni, Salum Mwalimu amesema kuwa kuondoka kwa mtu mmoja ndani ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) hakuathiri chochote kwani bado umoja huo uko imara.

Ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na Dar24 Media, ambapo amesema, Maulid Mtulia alipokuwa UKAWA walimpigania kwa nguvu zote bila kujali tofauti za itikadi zao za vyama, dini wala kabila mpaka aliposhinda Jimbo la Kinondoni katika uchaguzi mkuu uliopita.

Aidha, akizungumzia mikakati yake aliyojiwekea kama atashinda nafasi hiyo ya ubunge kwa jimbo la Kinondoni, amesema kuwa kuna tatizo kubwa sana la kujaa maji sehemu mbalimbali za jimbo hilo, makazi holela na bomoa bomoa, hivyo hizo ndizo changamoto atakazo anza nazo ili kuinusuru jamii na majanga ambayo yamekuwa yakijitokeza mara kwa mara.

Ameutaja mkakati mwingine aliouwekea kipaumbele ni kushughulikia mfuko wa fedha wa vijana na wanawake ambao utasaidia kuondokana na umasikini na kuongeza kipato cha mmoja mmoja katika familia.

Video: Acheni propaganda za nani hapigi kura- Salum Mwalimu
Kesi ya Aveva, Kaburu yaahirishwa tena

Comments

comments