Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu na Taasisi za Haki za Binadamu na Maendeleo ya Kiuchumi ya Watu wenye Ulemavu, kimeeleza kusikitishwa sana na kitendo cha Jeshi la Polisi kutumia nguvu kubwa wakati wakizuia maandamano ya watu wenye ulemavu Juni 16, 2017 katika eneo la Posta Jijini Dar es salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, Anna Henga, amesema kuwa kitendo hicho si cha kiungwana kwani walemavu hao wana haki ya kuandama kudai haki yao ya msingi, amesema walemavu ni moja kati ya makunndi maalumu katika jamii ambayo yanastahili heshima na ulinzi mkubwa wenye kuhakikisha usalama na mazingira mazuri .

 

Liverpool Kumnasa Mohamed Salah
Nikki wa Pili Kama Jay Z, Aweka Wazi Uwezo Wake Uliomshangaza P-Funk