Msanii wa muziki wa bongo fleva nchini Linah Sanga ambaye amekuwa kimya kwa muda mrefu kwa kile kilichodhaniwa kuwa alikuwa akilea mtoto wake ambaye amezaliwa mwishoni mwa mwaka jana.

Kupitia ukimya huo amekuja na wimbo wake mpya aliomshirikisha Rachel ujulikanao kama ”Same boy” wimbo huo umebeba maudhui kama ya  wimbo wa Same girl ulioimbwa na R-Kelly akiwa amemshirikisha  Usher Raymond mnamo mwaka 2009.

Nyimbo hizo zikiwa na maudhui yanayofanana ambapo katika wimbo wa Linah na Rachel, ”Same boy” wote wakiwa wanatamani kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwaanume mmoja, huku maudhui katika wimbo wa Same Girl ulioimbwa na R-Kelly na Usher Raymond ukielezea jinsi wanaume hao walivyokuwa wanamzungumzia msichana mmoja waliojihusisha nae katika mapenzi.

Kutazama video ya Linah bonyeza link hapo chini.

Gari la msafara wa Rais Kabila lapata ajali, laua
Rais wa Fifa ndani ya Tanzania

Comments

comments