Mbunge wa Singida Mashariki na Rais wa TLS, Tundu Lissu amesema kuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia Na Maendeleo (CHADEMA), Dkt Vicent Mashinji amepata dhamana ya Polisi huku akidai kwamba kiongozi huyo ameambiwa aripoti kesho ambapo hadi sasa hawajajua anatakiwa kuripoti kwa RPC au kwa nani.

Ameyaasema hayo mapema hii leo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari na kueleza kuwa baadhi ya viongozi wa Chadema waliokuwa wamekamatwa siku za hizi karibuni ni pamoja na Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho Waziri Mkuu wa Zamani, Edward Lowassa na Mbunge wa Kawe Halima Mdee.

“Viongozi wetu wamekuwa wakikamatwa kamatwa bila sababu ya msingi, maana kwa sasa hivi haipiti wiki utasikia kiongozi wa Chadema amekamatwa, hali hii sio nzuri hata kidogo kwenye chama chetu,”amesema Lissu.

Aidha, Lissu amemtupia lawama Rais Dkt. John Magufuli kwa kusema kuwa anagawa madaraka kwa upendeleo, hivyo amemuomba kuacha kufanya hivyo kwani atajenga fikra mbaya kwa wananchi.

Hata hivyo, Lissu hali ya kisiasa hapa nchini inavyokwenda na kusema kuwa kuna baadhi ya vyama vya upinzani hapa nchini ambavyo ni visaliti huku akitolea mfano kwa Chama cha Wananchi (CUF) upande waLipumba.

Magazeti ya Tanzania leo Julai 18, 2017
Video: Ndege ya Serikali kusafirisha mwili wa mke wa Dkt. Mwakyembe

Comments

comments