Timu ya Chelsea ambao walikuwa wenyeji wa pambano la mchezo wa Ligi Kuu ya England katika uwanja wa Stamford Bridge, London dhidi ya Liverpool wameshindwa kuibuna washindi baada ya kukubali kichapo cha bao 1 – 2.

Liverpool walijipatia mabao hayo mawili kipindi cha kwanza kupitia kwa Dejan Lovren(dakika ya 17) na Jordan Henderson(dakika ya 36) na kufanya mchezo huo mpaka mapumziko matokeo yakiwa goli 0 – 2 Liverpool wakiwa mbele.

Katika kipindi cha pili cha mchezo huo Chelsea walionekana kulishambulia vilivyo lango la Liverpool na kubahatika kupata goli moja dakika ya 61 kupitia kwa Diego Costa na kufanya mchezo huo kumalizika kwa matokeo ya 1 – 2, Liverpool wakitoka kifua mbele.

Hizi hapa highlights za mchezo huo.

 

Barnaba aeleza jinsi Mastaa walivyoukataa wimbo wa ‘Yule’ uliomtoa Ruby
Video: Mtanzania anayeimba Taarabu Canada amekuja na hii 'Msaliti'