Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Lulu Diva ambaye kwasasa anatamba na wimbo wake wa ‘Nilegeze’ amesema kuwa yeye hajatelekeza mtoto wala hana mtoto.

Lulu Diva amejibu tuhuma hizo lilizotolewa na mwanamuziki mwenzake TID katika mitandao ya kijamii akidai kuwa kuna wadada wanajipendezesha, wananunua hadi nywele za mamilioni lakini wametelekeza watoto wao.

“Amepitiwa tu, yeye ni kaka yangu wala sitajibizana naye kuhusu hilo, anapaswa ajitambue kuwa amekosea, siwezi kuwa na bifu naye kutokana na kitu alichosema.” amesema Lulu Diva.

Kupitia ‘Exlusive’ ya Dar24, Lulu Diva pia amemtaja Hamisa Mobetto kuwa miongoni mwa wadada wanaompa ushawishi wa kupambana kutokana na juhudi zake.

Bofya hapa chini kutazama zaidi

 

Chanzo cha moto Kanisa kuu la Notre Dame chatajwa, Rais aahidi kulijenga uypya
Hizi hapa nafasi za ajira kutoka makampuni 10 Tanzania

Comments

comments