Mkuu wa Wilaya ya Temeke Felix Lyaniva,leo ameongoza zoezi la kujitolea damu lililofanyika katika viwanja vya mwembe yanga jijini Dar es Salaam, amesema kuwa jumuiya kiislam ya Jai Jai imefanya kitendo kizuri na cha kuigwa.

Amesema hayo mapema hii leo jijini Dar es salaam, Lyniva ameongeza kuwa  damu haina ubaguzi wa kabila, dini wala rangi ya mtu kwa hiyo kila mtu anaweza kutumia.

Aidha, Lyaniva amewasihi madhehebu mengine kuiga mafano kwa jumuiya hiyo ya kiislam kwa kufanya kama walivyo jumuiya hiyo ya jai jai na kuongeza kuwa damu hiyo itawasaidia wagonjwa wa saratani ya damu na watu wengine wenye shida.

Hata hivyo, Lyaniva ameongelea suala la panyaroad na kuwaomba wazazi na walezi kufuatilia mienendo ya watoto wao ili wasije kujiingiza katika kundi hilo kwani polis wamejipanga kikamilifu

Magufuli amnyang’anya rasmi Sumaye shamba la Dar
Video: Sakaya atoboa siri na mwarobaini wa mgogoro wa CUF, ‘ni mgogoro binafsi’