Aprili 25 ya kila mwaka, ni siku ambayo maadhimisho ya malaria hufanyika duniani kote, ambapo Serikali ya Tanzania inatarajia kuungana na nchi zingine duniani kwenye kuadhimisha ya siku hiyo.

Maadhimisho hayo ya kitaifa yatafanyika wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma huku Waziri wa Afya na Maendeleo ya Jamii akitarajiwa kuzindua ripoti ya hali ya Malaria nchini.

Akiongea jijini Dar es Salaam, Waziri Nyoni ambaye ni Mkurugenzi wa Miradi kutoka VectorWorks amesema kutakuwa na shamra shamra mbali mbali kuanzia Aprili 22, 2018 kabla ya kufikia kilele cha maadhimisho hayo.

VectorWorks ni mradi wa miaka mitano wa kupamba na malaria hapa nchini umefadhiliwa na Shirika la Misaada la Marekani – USAID kupitia Mfuko wa Rais wa Marekani wa kudhibiti malaria na kuratibiwa na John Hopkins Center for Communications.

‘Sisi kazi yetu ni kuhakikisha hali ya ugonjwa wa malaria inapungua. Kwa sababu hiyo, tumekuwa na zoezi endelevu la kugawa vyandarua vyenye dawa ya muda mrefu kwa kila kaya hapa nchini.

Amesema vile vile, wanatumia vituo vya afya kuwafikia walengwa wakuu ambao ni akinamama waoenda kliniki na watoto wenye umri chini ya mwaka mmoja.

Akina mama wanaonza kliniki ni lazima wapatiwe chandarua chenye dawa ya muda mrefu bure. Hii njia bora ya kujikinga na mbu waenezao malaria. Vile vile tunafanya kazi kwa kushirikiani na

Serikali kupitia Wizara ya Afya kitengo cha kupamba na Malaria nchini ambao wamekuwa wakipuliza dawa yenye viatilifu kwenye maeneo yenye masalia ya mbu, imepiga hatua kubwa

kupunguza malaria hapa Tanzania kwa hivyo natoa wito wangu kwa kila Mtanzania kuhakikisoni.

Kauli mbiu ya mwaka huu ni mimi natokomeza malaria, wewe je?

Wafuasi wa vyama vya upinzani waendelea na maandamano nchini Madagascar
Usambazaji wa gesi ya bei nafuu kuanza jijini Dar