Kaimu Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF) na Mbunge wa Jimbo la Kaliua, Magdalena Sakaya amesema kuwa Katibu Mkuu wa Chama hicho ndio tatizo kubwa la mgogoro ulikiyumbisha chama hicho.

Ameyasema hayo jijini Dar es salaam wakati akizungumza na Dar24 Media, ambapo amesema kuwa kama Maalim Seif angemsikiliza haya yote yanayoendelea yasingeweza kutokea.

Amesema kuwa mgogoro wa chama hicho ni wa kikatiba, hivyo Maalim Seif aliamua kuivunja Katiba kwa makusudi ili aweze kutimiza kile alichokuwa akikihitaji.

“Chanzo cha mgogoro huu ni Maalim Seifu kuivunja Katiba kwa maslahi yake binafsi, hakutaka kunisikiliza ndio maana leo tumefikia hapa,”amesema Sakaya

Serikali yatenga Bilioni 23 mkoani Pwani
Video: Kiongozi Chadema anyongwa, Sombasomba nyingine wauza 'unga' inakuja

Comments

comments