Serikali imesema agizo la Rais Magufuli akiwa Mwanza kuhusu kutokuwahamisha wafanyabiashara wadogo(Machinga) kutoka maeneo walipo ni endapo hakuna maeneo yaliyotengwa kwa ajili yao.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi, Selemani Said Jafo wakati akijibu swali Bungeni Dodoma leo Novemba 3, 2016. Jafo amezitaka Halmashauri zote nchini kutenga maeneo kwajili ya Machinga kutokana na umuhimu wao wa kukuza kipato na ajira.

Aidha amewataka Machinga kuzingatia sheria na kuhakikisha wanafanya biashara zao katika maeneo yaliyotengwa ili kuepusha usumbufu.

Video: Alichosema Mbunge Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ Bungeni leo

Aaron Ramsey: Tutakua Wa Kwanza Kuwafunga Spurs
Wachina Wakaribia Kuinunua Southampton FC