Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole amesema kuwa maendeleo si kutukanana majukwaani bali ni kubadilisha maisha ya watu.

Ameyasema hayo katika kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani, ambapo amesema kuwa siasa si ugomvi bali ni kushughulika na maisha ya watu.

Amesema kuwa maendeleo hayana chama hivyo hakuna haja ya kutukanana hivyo ni bora kujikita katika kushughulikia changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi.

Tunakagua Leseni sio vyeti- Kamanda Muslim
Lugola amtwisha zigo jingine Inspekta Sirro

Comments

comments