Leo Desemba 13, 2016 Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi, Rais John Pombe Magufuli ameongoza kikao cha Halmashauri kuu ya Taifa ya chama hicho.

Katika kikao hicho kilichofanyika Ikulu, jijini Dar es salaam, Rais Magufuli amepokea  taarifa ya Tathimini ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, ambapo mara baada ya kuitafakari taarifa hiyo Halmashauri Kuu ikaamua kufanya mabadiliko mbali mbali ikiwa ni pamoja na kupunguza idadi ya wajumbe wa vikao na idadi ya vikao vya chama katika ngazi mbali mbali ili  kuongeza muda wa viongozi wa chama kufanya kazi za chama kwa Umma badala ya kutumia muda mwingi katika vikao.

Aidha, Rais Magufuli amefanya teuzi katika chama hicho kujaza nafasi mbali mbali ndani ya Sekretariete ambazo zilikuwa wazi kutokana na waliokuwa wakizishikilia kupewa majukumu mengine ya kiserikali

Serikali yazindua mpango kazi kupinga ukatili kwa wanawake na watoto
Yahaya Ajiwekea Malengo CAF