Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli, amesema kuwa Ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) aina ya Bombadier Q400, iliyokuwa ikishikiliwa nchini Canada imekwisha achiwa huru.

Rais Magufuli ametoa taarifa hiyo leo Desemba 12, 2019, Jijini Mwanza, wakati akifungua semina ya Wajumbe wa Halmashauri Kuu Taifa (NEC) ya Chama cha Mapinduzi (CCM).

“Kwanza kwa taarifa tu Ndege yetu iliyokuwa imeshikwa Canada imeachiwa, mtatangaziwa tarehe ya kuipokea na mtaipokea hapa hapa Mwanza” amesema Rais Magufuli.

Taarifa za kukamatwa kwa Ndege hiyo zilitolewa siku ya Novemba 23, 2019, Ikulu ya Chamwino, Jijini Dodoma na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi…, Bofya hapa kutazama

Benki yaonya wafuasi wa Bobi Wine wanaoandika fedha
Kila mfungwa aliyesamehewa Katavi amepewa Ardhi hekari 5