Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli amesema serikali yake imejipanga kuleta maendeleo kwa wananchi na kuongeza kuwa nchi ilipokuwa imefikia ilkuwa na hali mbaya.

Ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Ikulu Jijini Dar es salaam na kusema kuwa rushwa ilikuwa imeshamili kila kona na ndiyo iliyokuwa inaitafuna nchi.

Mbali na hayo Rais Magufuli amezungumzia mafanikio mbalimbali yaliyopatikana katika kipindi chake cha mwaka mmoja toka aingie madarakani ikiwemo kuongezeka kwa mapato kutoka bilioni 800 mpaka makusanyo ya shilingi trilioni 1.5 kwa mwezi.

Amesema kuwa Bajeti ya mwaka 2016 ya trilioni 29.5 iliyotenga asilimia 40 kwenye miradi ya maendeleo imekuwa yenye mageuzi makubwa ukilinganisha na bajeti ya miradi hapo nyuma mabayo ilikuwa asilimia 26 tu.

Pamoja na hayo Rais magufuli amesema kuwa Serikali imeagiza ndege nyingine mbili zinategemewa kufika nchini mwanzoni mwa mwaka 2018 ili kuboresha sekta ya utalii nchini.

Akizungumzia uundwaji wa serikali amesema mategemeo yake katika serikali aliyoiunda imefanikiwa kwa kuwa Baraza aliloliunda la watu wachache limekuwa la mafanikio makubwa na hili limetokana na ushirikiano mkubwa wa mawaziri wake.

Aidha Rais Magufuli amevitaka vyombo vya habari nchini kubadili mtazamo wao katika uandishi wao wa habari na kuandika habari ambazo zina maslahi kwa Taifa na kuwahakikishia waandishi wa habari kushirikiana nao kwa kuwa anatambua kazi nzuri wanayoifanya.


Ndalichako atoa matumaini mapya kwa wanafunzi kuhusu Mkopo
Video: Mambo 16 aliyosema Rais Magufuli katika mahojiano na waandishi Ikulu