Leo Oktoba 5, 2016 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ametembelea Gereza la Isanga mjini Dodoma na kumuagiza Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana kuchunguza ni kwa nini Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dodoma, Antonino Kilumbi amekwenda kutengeneza madawati kwa watu binafsi  badala ya karakana ya Magereza kama  ilivyokusudiwa na Serikali.

Majaliwa amesema Magereza mkoa wa Dodoma ilipewa sh. milioni 24 na Serikali ili kutengeneza madawati 480 na kila moja lilitakiwa kugharimu sh. 50,000 lakini uongozi wa gereza hilo ulitengeneza madawati hayo kwa watu binafsi ambapo dawa moja limegharimu sh. 70,000.

“Nimesikia kwamba mnawachangisha askari kiasi kilichoongezeka kwenye utengenezaji wa madawati hayo. Ni marufuku askari kutoa fedha mifukoni mwao kulipia shughuli za Serikali,” –  Waziri Mkuu Majaliwa

Bofya hapa kutazama video

Video: Wizi wa madalali sasa bhaasi - Waziri Lukuvi
Video: JPM ashtukiza tena uwanja wa ndege Dar, waliomdanganya kuwajibishwa