Leo June 28, 2018 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ametoa agizo zito kwa watumsihi wa Halmashauri ambapo amesema kuanzia leo gari zote za Serikali baada ya muda wa kazi zinatakiwa kurudi halmashauri na kumpa kazi mkurugenzi kusimamia suala hilo.

Pia amepiga marufuku kwa mtumishi yeyote wa serikali anayetumia gari za serikali kulaza gari hiyo nyumbani kwake.

”Kuanzua leo gari zote za sereikali zote, zote baada ya miuda wa kazio ziwe kjwenye yard ya mwandisi kama kuna gari itakuwa nje ya kituo mkurugenzi atakuwa anajua na ni kwa kazi maalumu ya serikali na haturuhusu mtu yeyote kukaa na gari ya serikali nyumabni kwake” Amesema Majaliwa.

Waziri Mkuu, ameongea hayo leo pindi alipokuwa akihutubia jijini Dodoma wilayani Bahi ambapo pia ameagiza watumishi wote wanaoishi nje ya eneo la kazi wawe wamehamia.

Amwaagiza watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Bahi mkoani Dodoma wanaoishi nje ya eneo lao la kazi wawe wamehamia ifikapo July 30, mwaka huu.

Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Juni 29, 2018
Nywele za kiafrika zawa maonesho kwa vinyozi wa Urusi

Comments

comments