Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amewataka ndugu na jamaa wa familia wa Ruge kuwa na Umoja hasa katika wakati huu wa kipindi cha msiba wa Ruge Mutahaba.

Ameyasema hayo jijini Dar es salaam mara baada ya kuwasili nyumbani kwa baba mzazi wa Ruge Mutahaba, ambapo amewataka ndugu Jamaa na marafiki wa familia hiyo kuwa wavumilivu hasa katika kipindi hiki kigumu.

”Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli iko pamoja nanyi wakati wote wa msiba huu, hivyo rais anawapa pole sana na atakuja muda wowote, atakapo maliza majukumu mengine,”amesema Majaliwa

Video: Ruge alinisaidia kabla hata ya kuanza kazi CloudsFm- Fredy
Kusaga anena kuhusu Ruge Mutahaba

Comments

comments