Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema kuwa Tanzania siyo lango la kupitishia dawa za kulevya kwenda nchi za nje hivyo ameagiza ulinzi uimarishwe katika mipaka yote ya nchi na kuwa wale watakaobainika watachukuliwa.

Majaliwa amesema hayo wakati akizungumza na watumishi wa kituo cha forodha cha Kasumulu kilichopo mpakani mwa Tanzania na Malawi wilayani Kyela, amesema kuwa kunatabia ya baadhi ya watu wasiokuwa waaminifu kuitumia Tanzania kama njia ya kupitisha dawa za kulevya kwa ajili ya kupeleka nchi za  Afrika ya Kusini, Malawi na Zambia.

“Endeleeni kufanya upekuzi wa kina wa magari, watu na mizigo yote yote katika mipaka yetu. Tanzania siyo lango la kupitishia dawa za kulevya na Serikali haitakubaliana na jambo hilo.”

Aidha, Majaliwa amewataka viongozi hao kuhakikisha biashara zote za magendo zinazofanyika mipakani, zikiwemo za kubadilisha fedha zinadhibitiwa kwa kuwa zinaikosesha Serikali mapato.

Hata hivyo, ameongeza kuwa ni vema yakawepo maduka ya kubadilishia fedha katika maeneo hayo ili kudhibiti biashara hiyo ambayo kwa sasa inafanywa kimagendo huku Serikali ikikosa kodi.

 

Tanzania yaombwa msaada na Uturuki
Sakaya amshukia Maalim Seif, ahofia uwezo wake wa kufikiri