Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amezindua mradi wa uboreshaji miundombinu ya umeme jijini Dar es Salaam ili kunaondoa adha zilizokuwepo awali kutokana na kukatika umeme mara kwa mara.

Wakati akizungumza na wananchi na viongozi mbalimbali waliohudhuria uzinduzi wa mradi huo uliofanyakoa leo Novemba 16, 2016 kwenye Ofisi za TANESCO, Mikocheni jijini, amewataka wakazi wa Jiji la Dar es Salaam kutumia fursa ya uwepo wa umeme huo wa uhakika kwa kuanzisha viwanda vidogo na vikubwa ili waweze kujiongezea kipato.

“Hivi sasa tumepata umeme wa uhakika, fanyeni kazi kwa bidii ili mfaidi matunda ya kuwepo kwa umeme huo. Serikali inategemea kwamba sasa wananchi mtaanzisha na kukuza viwanda vidogo vidogo na vikubwa, biashara zitapanuka na kilimo bora huko vijijini kitaongezeka,” – Majaliwa.

Video: 'Hatutaki mgao wa umeme' - Waziri Muhongo
TFF Yampiga Marufuku Christopher Mahanga