Polisi kanda maalum ya Dar es salaam leo tarehe 12 Agosti 2016 imetoa ripoti ambapo jeshi hilo limeeleza kukamatwa kwa majambazi hatari wanne.

Akitoa taarifa hiyo Naibu kamishna wa Polisi kanda maalum ya Dar es salaam, DCP Hezron S. Gyimbi pia ameeleza kuwa Jeshi hilo limekusanya zaidi ya bilioni moja kupitia tozo za makosa ya usalama barabarani kuanzia tarehe 29/072016 hadi 11/08/2016

  • Idadi ya magari yaliyokamatwa 39,280
  • Idadi ya Pikipiki zilizokamatwa 2,382
  • Daladala zilizokamatwa 16,739
  • Magari mengine (binafsi na malori) 22,541
  • Bodaboda waliofikishwa mahakamani kwa kosa la kutokuwa na Helment na kupakia mishkaki(abiria zaidi ya mmoja) 12

Hivyo jumla ya yaliyokamatwa ni 41,662 na kufanya jumla ya tozo zilizopatikana kuwa ni shilingi 1,249,860,000/=

Chid Benz: Huwezi Kunifananisha na Joh Makini
Mpinga Cup Yazinduliwa Wilaya Ya Ilala