Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Simon Sirro amesema kumekuwa na mafanikio mengi ya ukamataji wa silaha nyingi, huku akieleza kuwa jambo kubwa zaidi ni ukamataji wa Majambazi wanaotumia silaha kufanya uhalifu.

Sirro amesema hayo leo Desemba 30, 2016 ambapo ameeleza kuwa uhalifu mwingi umepungua kwa ushirikiano mzuri wa wanachi na idara zote za polisi na vyombo vya dola, amesema matarajio makubwa ni kuhakikisha uhalifu unapungua zaidi kati ya asilimia 10 hadi 15 katika mwaka 2017 ili wananchi wa Dar es salaam wafanye shughuli zao za kimaendeleo kwa amani na uhuru zaidi.

Majimaji FC Waivimbia Azam FC
Mark Hughes aupeleka ubingwa wa PL anfield kwa masharti