Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson amesema kuwa wabunge wanawake wameamua kuanzia kampeni ya nyumba ni choo kwaajili ya kuwasaidia watoto wa kike.

Ameyasema hayo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na Dar24 Media wakati wa hafla iliyofanyika kwaajili ya kuchangia ujenzi wa vyoo katika shule za sekondari za wasichana iliyofanyika jijini Dar es salaam.

Dkt. Ackson amesema kuwa kumsaidia mtoto wa kike ni kumpa fursa ya kuweza kufanya vizuri katika masomo yake darasani.

“Unajua ukimuweka sawa mwanafunzi wa kike katika hadhi yake na mazingira aliyonayo yanauwezo mkubwa sana wa kumuwezesha kufika mbali katika elimu yake, hivyo wito wangu naomba tuwasaidie watoto wa kike ili waweze kufikia malengo na ndoto zao,”amesema Dkt. Tulia

 

Video: Anna Makinda awafunda wabunge
Marekani yasitisha kutoa misaada kwa Palestina