Baraza la Habari Tanzania limetangaza majina ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali watakao wania tuzo za Umahiri za Uandishi wa Habari Tanzania (EJAT), baada ya jopo la majaji waliokuwa wakipitia kazi za waandishi hao kumaliza kazi na kukabidhi jumla ya majina 66 ya waandishi watakaowania tuzo hiyo.

Akitangaza majina hayo, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya EJAT 2016, Kajubi Mukajanga amsema jumla ya kazi 810 ziliwasilishwa EJAT 2016 ikiwa ni ongezeko la kazi 232 kulinganisha na kazi 568 zilizowasilishwa mwaka 2015.

“Halii hii ni mwelekeo mzuri kwa wanahabari wengi zaidi, wanatambua na kuthamini EJAT kama kipimo kizuri cha umahiri wa uandishi wa habari,” amesema Mukajanga.

Hata hivyo, ameitaja kamati ya maandalizi ya EJAT ni Tanzania Media Foundation (TMF), Taasisi ya Vyombo vya Habari ya Kusini mwa Afrika tawi la Tanzania (MISA-Tan), Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT), Haki Elimu, AMREF, ANSAF, BEST-Dialogue na SIKIKA, Kamati ya Maandalizi ya EJAT inayoongozwa na MCT.

Mhagama amtaja mgeni rasmi sherehe za Muungano
Wawekezaji kutoka Misri watua nchini, waahidi kujenga kiwanda kikubwa