Bendi ya muziki ya Major Lazer ya Marekani, imeendelea kuwapa mashavu wasanii wa Afrika, ambapo hivi sasa wameachia ‘Tied Up’ wakiwashirikisha Mr. Eazi na Raye.

Video ya ‘Tied Up’ ni  ya tatu kufanywa na kundi hilo kwa kushirikiana na muongozaji Adriaan Louw wa Afrika Kusini.

Ngoma hii imeachiwa ikifuata mkondo wa ‘Orkant/Balance Pon It’ aliyoshirikishwa staa wa Afrika Kusini, Babes Wodumo na ‘All My Life’ aliyoshirikishwa  Burna Boy.

Kundi hili ambalo hivi sasa limeonesha kulimulika kwa jicho la tatu bara la Afrika, limeachia pia Afrobeats Mix mpya ambayo ina wasanii wa Afrika kwa lengo la kuzipaisha kwenye majukwaa yao ya kimataifa.

Mfululizo wa ushirikiano huo unaambatana na ziara yao ya kwanza barani Afrika inayoendelea kwa kuzitembelea Afrika Kusini, Malawi, Kenya na  Uganda; wakitarajia pia kushiriki kampeni ya kutokomeza ujangili barani Afrika kwa kushirikiana na taasisi ya Veterans Empowered to Protect African Wildlife (VETPAW).

Fastjet Tz yapiga moyo konde msaada wa kifedha kusitishwa
Video: Beyonce auwashia moto mchepuko wa Jay Z

Comments

comments