Kundi la Major Lazer limeachia ngoma mpya ‘Orkant/Balance Pon It’ na kumpa shavu msanii wa Afrika Kusini, Babes Wodumo.

Audio ya ‘Orkant/Balance Pon It’ imeambatana na video mpya iliyofanywa kwa ushirikiano kati ya Major Lazer na muongozaji wa Afrika Kusini, Adriaan Louw.

Dubai ndilo eneo ambalo video ya ngoma hii imechukuliwa.

Hii ni video nyingine ya kundi hilo ambayo imemshirikisha msanii wa Afrika na muongozaji wa Afrika.

Awali kundi hilo liliachia ‘All my Life’ waliyomshirikisha Burna Boy wa Nigeria na video yake pia iliongozwa na  Adriaan Louw.

Hivi karibuni, Major Lazer pia walizindua Afrobeats Mix mpya, yenye mchanganyiko wa nyimbo toka barani Afrika na kutumia jukwaa lao la kimataifa kuonesha uwezo wa wasanii wa Afrika.

Aidha, kundi hilo pia litazuru nchi tano za Afrika kuanzia Oktoba mwaka huu. Nchi hizo ni Afrika Kusini, Malawi, Kenya, Ethiopia na  Uganda.

Breaking News: Madereva 50 wa Uber wanyang'anywa magari
Rais Magufuli afanya uteuzi mwingine NSSF

Comments

comments