Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, January Makamba amewataka wananchi kuepukana na uhalibifu wa mazingira kwani kufanya hivyo kutasababisha kutokea kwa majanga makubwa.

Ameyasema hayo jijini Dar es salaam wakati wa ziara ya ukaguzi wa ujenzi wa kingo za fukwe za bahari zilizopo Kigamboni na Ocen road.

Amesema kuwa ni bora wananchi wakashirikiana kulinda mazingira ili kujikinga na majanga ambayo yamekuwa yakisababishwa na uhalibifu huo.

“Uhalibifu huu wa mazingira umeanza kuonekana sehemu mbalimbali za nchi, kwa hiyo ni wajibu wa kila mtu kulinda mazingira ili tuepukane na hili,”amesema Makamba

Magazeti ya Tanzania leo Januari 19, 2018
Video: Marekebisho ya sheria ya vyama vya siasa yaiva