Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema kuwa vikao vya masuala ya Muungano vinaendeshwa kirafiki kama ndugu wawili ambao wamekaa na kujadili mambo yao.

Ameyasema hayo jijini Dodoma wakati wa ufunguzi wa kikao cha Kamati ya Pamoja ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SMT) na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) kujadili masuala ya Muungano.

Amesema kuwa vikao hivyo vina mambo mengi mchanganyiko si sheria na katiba peke yake vinavyofanya kazi kuna mengine, consideration zingine zinabidi ziingie ili kupata njia sahihi ya kujadiliwa.

Kwa upande wake Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi alikabidhi kiwanja chenye ukubwa wa hekari 30 kilichopo kwenye eneo la mji wa Serikali Dodoma kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar bila gharama yeyote kama alivyoelekeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.

Awali Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, January Makamba amesema kuwa kikao hicho ni cha kawaida ambacho kimejadili masuala ya Muungano na kilitanguliwa na vikao vingine vilivyojumisha Makatibu Wakuu pamoja na Mawaziri.

Hata hivyo, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amekabidhi hati ya umilikiwa wa kiwanja hicho chenye ukubwa wa hekari 30 kilichopo mji wa Serikali Dodoma kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Iddi.

Kikao hicho cha Kamati ya Pamoja ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SMT) na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) kujadili masuala ya Muungano kilihudhuriwa na Mawaziri wa Serikali zote mbili pamoja na Makatibu Wakuu na Timu ya Wataalamu.

Video: Sio siri tena, biashara ya nguo za ndani zenye vigodoro yatikisa mjini
Mbunge wa Chadema apata ajali