Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameagiza kubomolewa kwa nyumba 36 ambazo zipo kwenye maeneo hatarishi ya mabondeni ikiwemo bonde la mto Msimbazi.

Makonda amesema hayo leo Machi 14, 2017  wakati alipo tembelea zilizokubwa na mafuriko katika Kata ya Buguruni kwa Mnyamani na Tabata, akiwa na vikosi vya ulinzi na usalama ambapo ameshuhudia maafa makubwa yakiwemo ya baadhi ya watu kupoteza mali pamoja na nyumba zao kujaa maji.

Aidha, Kufuatia mvua zilizoanza kunyesha katika maeneo mbali mbali jijini Dar es salaam, zimepelekea kuleta maafa ikiwemo kifo cha mtu mmoja kilichotokea eneo la Jangwani, pamoja na watu wengi kupoteza makazi, jambo ambalo limemgusa Makonda na kufikia uamuzi huo wa kuiomba Halmashauri ya Ilala kuanza zoezi hilo la ubomoaji mara moja.

Vile vile, Makonda amesema kuna watu ambao tayari wamelipwa pesa kuhama maeneo hayo lakini cha ajabu wengine hawajaondoka na wengine wamewapangisha watu wengine kwenye maeneo hayo hatarishi, jambo ambalo Serikali yake haiwezi kulikalia kimya, ambapo tayari ametoa agioa la kubomolewa kwa nyumba hizo.

Hata hivyo, amewataka wale ambao hawajahakiki taarifa zao kuhusu kupewa hifadhi baada ya nyumba zao kubomolewa wafanye hivyo kwa kwenda ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ilala kwa uhakiki huo.

Magazeti ya Tanzania leo Machi 15, 2017
Kamishna Malewa aipongeza Serikali ya awamu ya tano