Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amefanya ziara katika ofisi za Baraza Kuu la Waislam nchini (BAKWATA) na kukagua maendeleo ya ujenzi wa ofisi za kisasa zitakazo kuwa na ghorofa nne.

Aimefanya ziara hiyo ya ukaguzi wa ujenzi ili kujionea maendeleo ya Ofisi hizo ikiwa ni sambamba na kuongea na wafadhili wa ujenzi huo.aidha kwa upande wake injinia wa ujenzi huo, Hersi Said amesema kuwa ujenzi huo unaendelea vizuri na wamekamilisha ghorofa ya kwanza na kuahidi kuwa baada ya wiki mbili watakuwa watakuwa wamekamilisha ghorofa ya pili.

Aidha, Injinia Said amesema ujenzi huo unataraji kukamilika rasmi mwezi wa 6 mwakani na kuongeza kuwa ofisi hizo za kisasa zitakuwa na nguzo tano kama ilivyo Dini hiyo ya Kiislamu.

Hata hivyo ameongeza kuwa katika ofisi hizo zitakuwa na Ukumbi wa Mikutano, Maktaba, Kompyuta, na ofisi mbalimbali za Mufti, ofisi nyingine ya Sheikh Mkuu wa Mkoa, Katibu Mkuu wa BAKWATA, Kadhi, Baraza la Maulamaa, kumbi za wanawake na Studio.

Kwa upande wake, Makonda ameonesha kuridhishwa na hatua za ujenzi huo na kusisitiza kuwa atafurahi endapo ujenzi huo utakamilika kwa wakati ili ifikapo mwezi mtukufu wa Ramadhani mwakani Ofisi hizo ziwe zimekamilika.

Jaffo awataka watumishi ilala kufanya kazi kwa bidii
JPM aridhia ombi la Mkuu wa Magereza, amteua Dk. Malewa kuwa Kaimu Mkuu