Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda ameungana na Wasanii mbalimbali na kufanya ziara ya ukaguzi katika ujenzi wa Reli Mpya ya Standard Gauge.

Ziara hiyo imeanzia jijini Dar es salaam na kuishia Ruvu mkoani Pwani ambapo amewataka Wasanii hao kuwa mabalozi wa kuitangaza reli hiyo.

Makonda amewataka wananchi na wadau wa maendeleo kuunga mkono juhudi za maendeleo zinazofanywa na rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli

“Niwaombe Wadau wa Maendeleo tuendelee kumuunga mkono rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli kwa juhudi za kuiletea maendeleo nchi yetu,”amesema Makonda

Wananchi Njombe waipigia magoti Serikali, 'Tusaidieni Jamani'
Video: DC Mtwara aonya upotoshaji wa taarifa dhidi ya mauzo ya Korosho

Comments

comments