Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amewataka kina Baba wote waliotelekezwa na wake zao kujitokeza ili waweze kupatiwa msaada wa kupata haki zao.

Ameyasema hayo jijini Dar es salaam alipokuwa akisikiliza shida mbalimbali za kina mama waliotelekezwa na waume zao, ambapo amesema kuwa sheria ni msumeno hivyo kina baba waliotelekezwa na wake zao wajitokeze.

“Mpaka sasa kuna kina baba huwa wanakuja na watoto wadogo kulalamika kuwa wake zao wamewatelekeza, hivyo basi, milango iko wazi kuanzia sasa, nawaomba wajitokeze,”amesema Makonda

 

 

Magazeti ya ndani na nje ya Tanzania leo Aprili 10, 2018
Ndugai awashukuru wabunge, awaombea wasipitie machungu aliyoyapitia