Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam,Paul Makonda amewapa muda wa miezi 4 wafanyabiashara wadogo wadogo wa Soko Urafiki linalojulikana kama Mahakama ya Ndizi kuhama katika eneo hilo kutekeleza agizo la Mahakama kwa kuwa eneo hilo ni mali ya kiwanda cha urafiki.

Amesema hayo wakati akizungumza na wafanyabiashara hao ambapo amesema kuwa hawawezi kuhamishwa kama ilivyokuwa awali bali wanatakiwa kuhama baada ya miezi minne kupita na kusema wakati huo Serikali itakuwa imeshawaandalia eneo maalum la kwenda ili kuepukana na matatizo kama hayo.

“Mtafanya biashara kwenye hili eneo kwa muda wa miezi minne hamtaondolewa leo wala kesho kama ilivyokuwa imepangwa bali tumeongeza siku 120 lakini pia nimemuelekeza Mkuu wa Wilaya ya Ubungo tayari kuna eneo limepatikana, tunataka tukamilishe utaratibu wa uhalali wa lile eneo ili watu wakienda pale wasipate matatizo kama haya yanayojitokeza ya kufukuzana fukuzana.” amesema Makonda

Hata hivyo, Mkuu huyo wa Mkoa amesema kuwa katika eneo ambalo watapewa litakuwa limeboreshwa zaidi ili wafanyabiashara hao waweze kupata wateja wa kila aina kwa kudai kuwa walipo sasa wanawakosa baadhi ya wateja kutokana na miundombinu ya soko hilo kutokuwa rafiki kwa baadhi ya watu.

 

Video: Lissu afumua mapya Lowassa kutua Ikulu, Wakili amtosa Wema kesi tuhuma za bangi
Magazeti ya Tanzania leo Januari 11, 2018