Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda leo amekabidhi Computer za kisasa 50 zenye thamani ya zaidi ya Shilingi Milioni 170 kwa Manispaa tano za Mkoa wa Dar es salaam pamoja kwa ajili ya kurahisisha utoaji wa vibali vya ujenzi.
Katika mgawanyo huo kila Manispaa imepatiwa Computer nane (8) huku Ofisi ya Jiji wakipatiwa Computer tano (5) na Ofisi ya Mkoa wakipatiwa Computer tano (5) ikiwa ni ufadhili wa kampun ya ulinzi ya TAMOBA Company Ltd iliyomuunga Mkono mkuu huyo wa mkoa kutokana na kuhamasika na utendaji kazi wake mzuri 
Amesema kuwa Computer hizo zitawekewa Mfumo wa kisasa ujulikanao kama Dar Ardhi E.System utakaoziunganisha idara zote zinazohusika na utoaji wa vibali vya ujenzi (One stop Center) ili kurahisisha Mwananchi kupata kibali cha ujenzi ndani ya muda mfupi
 “Kazi yangu kubwa ni kupunguza mateso, malalamiko na kero za Wananchi dhidi ya masuala ya Ardhi, na namna mbili za kupunguza ni pamoja na kuwawezesha watendaji kuwa na nyenzo na vifaa vitakavyorahisisha kufanya kazi zao kisasa zaidi kuendana na kasi ya Rais wetu Dkt. .John Magufuli,”amesema Makonda 

Dkt. Mpango awaonya wanaokwepa mashine za EFDs
Makamba afanya ziara ya ukaguzi wa ujenzi wa kingo za fukwe jijini Dar