Leo Aprili 12, ,2019 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda ameahidi kuwapa wachezaji timu ya Serengeti Boys shilingi milioni ishirini kwa kila mchezaji.

Amesema ahadi hiyo itakamilika endapo wachezaji watashinda mechi mbili katika mchuano wa AFCON 2019 na kufuzu kuingia katimba mashindano ya kombe la dunia.

Amesema hayo leo katika hafla fupi ya ugawaji wa zawadi kwa askari waliofanya vizuri, askari walioumia wakiwa kazini na kwa wanawake waliofiwa na waume zao waliokuwa maaskari.

Tukio hilo limefanyika katika viwanja vya polisi Oysterbay jijini Dar es salaam ambapo sherehe hiyo inatarajiwa kuendelea jioni ya leo katika ukumbi wa Mlimani City.

Mashabiki wamvaa Lil Wyne kifo cha Nipsey Hussle
Video: "Chadema inazama, haiwezi shika dola, nikaona nihame" - Mbunge Marwa

Comments

comments