Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amewashukuru wananchi kwa kujitokeza kwa wingi katika zoezi la upimaji afya bure lililoanza septemba 24 na kuhitimishwa leo Septemba 27, 2016 katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam.

Makonda amewataka wale wote waliopata huduma hiyo ya bure kuyafanyia kazi majibu waliyopatiwa na madaktari, na wale ambao hawakufanikiwa wawasiliane na hosptali za serikali kwaajiri ya kuendelea na vipimo vingine na kuweza kutatua matatizo yao.

“Nawashukuru sana wananchi wa mkoa wa Dar es salaam na mikoa jirani kwa kujitokeza kwa wingi kuja kupima afya bure, zoezi limeenda vizuri ingawa hapo mwanzo kulikuwa na kasoro ndogo ndogo, pia jeshi la wananchi limetusaidia sana katika kuongeza nguvu za madaktari.” – Makonda.

Video: Zoezi la upandaji miti ni endelevu Wilaya ya Ilala - DC Mjema
Wenger Amkingia Kifua Sam Allardyce