Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda ameikubali nguvu kubwa walionayo walevi katika zoezi zima la ushangiliaji wa soka hapa nchini.

Leo akizungumza katika hafla fupi ya ugawaji zawadi kwa maaskari ameomba chama cha walevi kutoa ushirikiano mkubwa katika kuhamasisha mashumbulizi na watu kujitokeza kushangilia timu yaTaifa chini ya miaka 17.

Ameomba chama cha walevi kuunga mkono timu ya Serengeti Boys inayotarajia kuanza michuano ya AFCON siku ya Jumapili ya Aprili 14, 2019.

Aidha siku chache zilizopita Mkuu wa Mkoa alitoa dongo kwa Piere Mollel maarufu kama Piere Liquid aliyejipatia umaarufu kupitia unywaji pombe wake uliomfanya kuchangamsha na kufurahisha watu na kutoa mchango mkubwa kwa timu ya taifa kufuzu michuano ya AFCON 2019 kwa ushindi wa tatu bila dhidi ya Uganda.

Msikilize hapa.

Anusurika kifo baada ya kuchomwa visu mara 17 na mumewe
Mashabiki wamvaa Lil Wyne kifo cha Nipsey Hussle

Comments

comments