Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda ametangaza kumsimamisha kazi engineer Mkuu wa Mkoa wa Dar, Josephat Shehemba kwa kushindwa kusimamia majukumu yake vyema. Makonda ameeleza hayo jana Juni 27 2016 na amechukua hatua hiyo baada ya kuona uzembe na kutokuwajibika kwa Inginia huyo ambaye alikuwa hatimizi majukumu yake ipasavyo.

“Kwahiyo nimemuagiza RC wa mkoa wa Dar es Salaam nimemuandika barua kumsimamisha kazi Engineer mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam kwa kutotimiza wajibu wake wa kazi na kupoteza mabilioni ya fedha ambazo zingetusaidia kutengeneza barabara zetu, uchunguzi unaendelea kwa makandarasi wote waliojenga barabara chini ya kiwango watafikishwa katika vyombo husika– Paul Makonda

Video: Rais Magufuli Apata Pongezi Kutoka Jukwaa Huru la Wazalendo Tanzania
Kuwa Single Mama ni Baraka Kubwa Sana- Faiza Ally