Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amesema kuwa Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu aliyeko ziarani barani Ulaya, ametaka akirudi apelekwe katika hospitali ya Milembe iliyopo jijini Dodoma.

Ameyasema hayo jijini Dar es salaam wakati wa mkutano kati ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli na Wafanyabiashara pamoja na  wadau wa sekta ya madini, ambapo amewataka Watanzania kuwa wazalendo.

Amesema kuwa miradi mingi imekuwa ikitekelezwa na serikali ya awamu tano ya tano, hivyo Watanzania wanapaswa kuunga mkono juhudi zinazofanywa na rais Dkt. Magufuli.

Aidha, akizungumzia suala la Mbunge wa Singida Mashariki kupitia Chadema, Tundu Lissu, kuhojiwa katika kipindi cha HARD TALK kinachurushwa na shirika la utangazaji la BBC, ambapo Lissu alisema kuwa serikali ya Tanzania imekuwa ikikiuka misingi ya haki za binadamu na utawala bora, kitu ambacho kimezua mjadala mkubwa katika mitandao ya kijamii.

Video: Walimu wabovu waziponza shule za Umma
LIVE: Rais Magufuli akizungumza na Wachimbaji, Wafanyabiasha na Wadau wa Sekta ya Madini

Comments

comments