Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda ameagiza kukamatwa kwa tajiri mwenye asili ya kiasia, Ajay Zaverchande Chohan kwa tuhuma za kununua eneo la shule ya msingi mapinduzi iliyopo kata ya Kigogo, Wilaya ya Kinondoni.

Ametoa agizo hilo wakati wa hafla ya uzinduzi wa upauaji majengo ya ofisi 42 za Walimu zinazojengwa kwa misaada ya hiari ya wadau wa elimu.

Aidha, amechukua hatua hiyo mara baada ya Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Fina Makocha kumweleza mkuu huyo wa mkoa kuwa moja ya changamoto kuwa ni pamoja na wananchi kuvamia eneo la shule.

“Haiwezekani mtu anunue eneo la shule kwa makusudi, polisi naomba mkamateni akaeleze vizuri ni kwanini alinunua eneo la shule, sasa hivi mtu anayeuza na anayenunua eneo la shule wote wakamatwe,”amesema Makonda

Taasisi za umma zatakiwa kutumia gesi
Video: Mbowe atema nyongo Siha, Jeshi la Polisi lamuwakia Kigwangalla