Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda  amemuweka ndani Mwenyekiti wa Serikali za Mitaa, Bakari Shingo wa Gongo la Mboto kufuatia tuhuma zilizotolewa na wananchi wa mtaa huo za kukusanya mapato huku akitumia risiti anazochapisha mwenyewe kinyume na maagizo ya halmashauri.

Makonda amefikia hatua hiyo ya kumuweka ndani Mwenyekiti huyo mara  baada ya kujiridhisha kwa kuwasikiliza wananchi na kumuagiza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Ilala, Salum Hamduni kumsweka rumande  mpaka upelelezi utakapo kamilika

Aidha, mjumbe wa Serikali za Mitaa wa Gongo la Mboto, Pili Seif amesema kuwa hiyo imekuwa ni tabia ya mwenyekiti huyo kwa muda mrefu na taarifa zimefikishwa kwenye mamlaka husika ikiwemo kwa Mkuu wa Wilaya, Sophia Mjema, Mkurugenzi Msongela Nitu na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.

Video: Makonda awataka watumishi kubandika majukumu yao kwenye milango yao

Makonda azidi kuwahukumu wenyeviti, amburuza mwingine rumande
Video: DC Lyaniva aitaja mikakati kuiboresha Temeke