Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda ametembelea na kutoa pole kwa Familia ya Wastaafu ya Edward Bejumula na Stella Bejumula walioteseka kwa miaka sita bila makazi baada ya kudhulumiwa nyumba yao waliyojenga baada ya kustaafu.

Makonda amewatembelea wastaafu hao na kuwapatia Msaada wa vitu mbalimbali ikiwemo Mchele, Unga, Sabuni, Ngano, Mafuta, Nyama, Viazi, Maharage, Sukari, Vitunguu, Ndizi, Nyanya kwa ajili ya matumizi ya nyumbani baada ya familia hiyo kupoteza Mali zote,

Aidha, amesema kazi ya kutafuta haki ya wastaafu hao inaanza mara moja kwa kuwahoji watu wote waliohusika na sakata hilo.

“Kazi hii ya kutafuta haki ya wastaafu hawa inaanza mara moja, haiwezekani watu wafanyekazi kazi kwa miaka yote halafu watu fulani tu waje kufaidi jasho la wastaafu,”amesema Makonda

Hata hivyo, kwa sasa wastaafu hao wanaishi kwenye nyumba ya mfadhili mmoja aliejitolea kuisaidia familia hiyo ambapo Makonda amemshukuru kwa moyo alioonyesha.

Magazeti ya Tanzania leo Januari 28, 2018
Sumaye: Mzanzibar yeyote anaruhusiwa kugombea Tanzania Bara