Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amepokea ugeni wa Wanajeshi wa Jeshi la Maji kutoka Nchini China waliokuja kwa lengo la kuimarisha mahusiano ya kijeshi ambapo amesema kuwa atandelea na mikakati ya kudhibiti uingizwaji wa dawa za kulevya zinazoingizwa nchini kwa kutumia bahari ya hindi.

Aidha, katika mazungumzo hayo na kikosi cha Jeshi hilo amewasilisha ombi la kupatiwa Boti za kisasa zitakazotumiwa Jeshi la polisi katika kuimarisha doria kwenye mwambao wa bahari ya hindi ili kukomesha biashara za magendo ikiwemo ya dawa za kulevya na bandari bubu.

Kwa upande wake Kamanda wa Jeshi la Majini la China Real Admiral, Shen Hao amesema kuwa ombi la Mkuu wa Mkoa la kupatiwa Boti za kisasa watalitimiza na kueleza kuwa wataendelea kuimarisha mahusiano ya kijeshi baina ya Tanzania na China.

Magazeti ya Tanzania leo Agosti 18, 2017
Jafo aamuru mkandarasi aliyetelekeza mradi wa maji asakwe