Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amefanya ziara ya kukagua mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Mama na Mtoto uliopo Chanika Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam na kusema kuwa mradi huo unatarajiwa kukamilika mwezi Februari 2017, ambapo utasaidia kutoa huduma kwa wakazi wa eneo hilo na maeneo jirani.

Ameyasema hayo mara baada ya kufanya ziara ya ukaguzi wa ujenzi wa mradi huo unavyoendelea  katika hospitali hiyo iliyopo Chanika wilaya ya Ilala jijini Dar es salaam.                                                                                                                                                                                                                                                                                Makonda amesema kuwa, Hospitali hiyo itakuwa na vitanda takribani 160 na uwezo wa kuhudumia zaidi ya wagonjwa 1000 kwa siku, huku kukiwa na vyumba viwili vya upasuaji vyenye uwezo wa kuhudumia wagonjwa wanne kwa kila chumba kimoja, ameongeza kuwa kutakuwa na watumishi zaidi ya 150 ambao watakuwa wanaishi hapohapo.

Aidha, Makonda amewaomba wafadhili wa mradi huo ambao ni Shirika la Maendeleo kutoka  Korea ya Kusini (KOICA), kusaidia upatikanaji wa mradi mwingine kama huo katika Wilaya za Ubungo na Kigamboni ambapo utaweza kusaidia wakazi wengi walio nje ya mji kupata huduma za afya kiurahisi zaidi.

Mradi huo wa  Hospitali ya Mama na Mtoto kwa Chanika unataraji kugharimu kiasi cha shilingi bilioni 8 na milioni 800, huku endapo kama miradi ya Ubungo na Kigamboni ikifanikiwa itagharimu zaidi ya shilingi bilioni 17.

Video: Magufuli atishia kumtumbua Waziri, Asema machinga wasisumbuliwe, Mama Salma pasua kichwa...
Kenya: Mgomo wa madaktari wapelekea vifo 8; wagonjwa 100 wa akili watoroka