Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda ametaja majina ya watu 13 ambao wanahitajika Kituo cha Polisi kuonana na Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Simon Siro siku ya ijumaa kwa ajiri ya kuhojiwa kuhusiana na matumizi ya mitambo ya kudukua filamu.

Makonda amtoa agizo hilo leo Aprili 19, 2017 katika maandamano ya wasanii wa filamu ambayo yaliratibiwa na wasanii wa filamu, ambapo amewataka wote wanaojihusisha na uuzaji wa CD za kutembeza mkononi pamoja na ‘wanabani’ miziki ya wasanii kuacha vitendo hivyo kwani vipo kinyume na sheria.

Amewataka wasanii kufurahia jasho lao kwani wanafanya kazi ya ziada katika kutekeleza kazi zao na kuanzia leo wasanii hao wataanza kunufaika nazo kwani sheria kali na utekelezaji utafuatwa.

 

Magazeti ya Tanzania leo Aprili 20, 2017
Madaktari 258 kuajiriwa na Serikali